• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Koeman ataja sababu ya kutimuliwa Everton

    (GMT+08:00) 2017-10-27 09:51:33

    Aliyekuwa meneja wa Everton Ronald Koeman amesema kuwa kushindwa kwake kumsaini mshambuliaji Olivier Giroud msimu huu kulichangia kufukuzwa kwake. Koeman alitimuliwa siku ya Jumamosi huku Everton wakiwa nafasi ya tatu kutoka mkiani. Anasema Giround, 31, alikaribia kukubali kuhamia Goodison Park. Everton ilimuuza mfungaji wao bora zaidi Romelu Lukaku, kwenda Manchester United mwezi Julai katika makubaliano ya kima cha pauni milioni 75.

    Everton ilitumia pauni milioni 150 kumununua mchezaji wa kiungo cha kati Gylfi Sigurdsson kwa pauni milioni 45, Kipa Jordan Pickford kwa pauni milioni 30 na mlinzi Michael Keane kwa pauni milioni 30 na mchezaji wa kiungo cha kati Davy Klaassen kwa pauni milioni 24.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako