• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yajitahidi kujenga jukwaa mpya ya ushirikiano wa kijeshi wa kimataifa

  (GMT+08:00) 2017-10-27 19:01:38

  Mkutano wa vyombo vya habari wa wizara ya ulinzi ya China umefanyika jana mjini Bejing. Msemaji wa wizara hiyo Bw. Ren Guoqiang amejibu masuala ya waandishi wa habari kuhusu uhusiano wa kijeshi kati ya China na Marekani na Russia. Amesema, China itajitahidi kujenga jukwaa mpya ya ushirikiano wa kijesh wa kimataifa na kusukuma mbele mambo ya ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya kijeshi upande ngazi ya juu zaidi.

  Hivi karibuni waziri wa ulinzi wa China Bw. Chang Wanquan alihudhuria mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa nchi za Asia Kusini Mashariki(ASEAN) na kueleza sera na msimamo wa China kuhusu sera ya kidiplomasia na majirani, na ushirikiano wa usalama wa kikanda. Amesema China itashirikiana na nchi za ASEAN kufanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja.

  "Jeshi la China litaendelea kuimarisha ushirikiano na mawasiliano na majeshi ya nchi mbalimbali hasa na nchi za Asia na Pasifiki, kuongeza maelewano na uaminifu ili kusukuma mbele maendeleo ya mazungumzo ya usalama ya pande mbalimbali. China pia imefikia makubaliano na nchi hizo kufanya mashauriano ya kiteknolojia ndani ya mwaka huu na kupanga muda wa mazoezi ya kijeshi kwa matokeo ya ushauriano huo."

  Kwenye mkutano huo, Bw. Chang pia amezungumza na mwenzake wa Russia Sergey Shoigu. Russia inaona majeshi ya China na Russia yameinua uhusiano wa pande mbili kwenye kiwango kipya. Msemaji wa wizara ya ulinzi Bw. Ren amesema, mwaka huu China na Russsia zitafanya juhudi kwa pamoja kwa ajili ya kuhimiza uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizi mbili uendelezwe kwa kina zaidi. Pande hizo mbili zimefanya mazungumzo mawili ya kimkakati, mikutano mitatu ya suala la kuzuia makombora na luteka mbili baharini. Pia majeshi hayo yanapanga kufanya luteka ya kuzuia makombora kwa kupitia kompyuta ndani ya mwaka huo.

  Rais wa Marekani Donald Trump atafanya ziara nchini China mwezi ujao. Bw. Ren amesema, hivi karibuni, majeshi ya China na Marekani yamepata maendeleo katika mazungumzo kati ya wakuu wa majeshi, mashauriano, mawasiliano, mazoezi ya kijeshi ya pamoja, utaratibu wa kuongeza uaminifu wa kijeshi. Pande hizo mbili pia zinatarajia kufanya mazungumzo ya sekta mbalimbali.

  "Tunapenda kushirikiana na Marekani kwa kuheshimiana, kuongeza hali ya kuaminiana, kutilia mkazo katika kufanyua mawasiliano na ushirikiano kwa kufuata hali halisi, na kudhibiti kwa kufaa maoni tofauti yaliyopo, ili kuendelea kuboresha maendeleo ya uhusiano kati yetu."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako