• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yakadiria kuwa bei ya bidhaa kubwa kupanda mwakani

    (GMT+08:00) 2017-10-27 19:17:27

    Ripoti ya robo mwaka kuhusu mustakabali wa soko la bidhaa kubwa iliyotolewa na Benki ya Dunia inaonesha kuwa bei ya bidhaa kubwa zikiwemo nishati na mazao ya kilimo inatazamiwa kupanda mwakani.

    Ripoti hiyo inasema kutokana na hali ya kutobadilikabadilika kwa mahitaji ya dunia, Jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta duniani na nchi nyingine zinazozalisha mafuta zinatazamiwa kutekeleza makubaliano ya kupunguza uzalishaji, mwaka huu bei ya mafuta ghafi duniani inatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 23.8 kuliko mwaka jana na kufikia dola za kimarekani 53 kwa pipa. Ripoti hiyo imekadiria kuwa bei ya mafuta ghafi itapanda kwa asilimia 5.7 na kufikia dola 56 kwa pipa.

    Benki hiyo pia imekadiria kuwa bei ya gesi asilia na makaa ya mawe itaongezeka kwa asilimia 23.7 mwaka huu, na kuongezeka kwa asilimia 4 mwakani. Bei ya mazao ya kilimo itapungua kwa asilimia 0.6 mwaka huu, na kuongezeka kwa asilimia 1.2 mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako