• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania asitisha uhamishwaji wa Wamasai kwenye eneo lenye machafuko

    (GMT+08:00) 2017-10-27 19:18:47

    Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Dk. Hamisi Kigwangalla leo ameamuru mamlaka za wilaya ya Ngorongoro kuacha kuwahamisha kwa nguvu watu wa kabila la Wamasai wanaoishi kwenye eneo lenye mgogoro lililo karibu na hifadhi huko Loliondo.

    Pia ameamuru kuachiwa kwa mifugo na mali nyingine za watu ambazo zilikamatwa wakati wa operesheni iliyoshuhudia nyumba kadhaa zikichomwa moto na mamlaka ya hifadhi ya wanayama pori, na kufanya mamia ya watu kukosa makazi.

    Zaidi ya hapo Dk. Kigwangalla amezipa mamlaka za wilaya na mkoa siku saba kuhakikisha kuwa mifugo na watu wanaoshikiliwa katika zoezi hilo wanaachiwa huru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako