• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yalaani shambulizi dhidi ya msafara wa walinda amani nchini Mali

    (GMT+08:00) 2017-10-27 19:22:08

    Wajumbe wa Baraza la usalama na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jana walilaani vikali shabulizi dhidi ya askari wa Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, na kusababisha vifo vya askari watatu na wengine wawili kujeruhiwa.

    Kwa mujibu wa taarifa shambulizi hilo lilitokea jana kwenye barabara kati ya Tessalit na Aguelhok nchini Mali, baada ya bomu kuwalipukia askari kutoka Chad waliokuwa wakisindikiza msafara kaskazini mwa Mali. Wajumbe wa baraza la usalama wameitaka serikali ya Mali kuchunguza shambulizi hilo na kuwafikisha wahusika kwenye mikono ya sheria.

    Kwa upande wake Bw. Guterres ametoa rambirambi kwa serikali ya Chad pamoja na ndugu wa askari waliouawa kwenye shambulizi hilo na kusisitiza kuwa mashambulizi yanayowalenga askari wa kulinda amani yanachukuliwa kama uhalifu wa kivita chini ya sheria ya kimataifa na kutaka wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako