• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kutekeleza jukumu la kulinda usalama wa meli kwenye eneo la bahari ya Somalia

    (GMT+08:00) 2017-10-27 19:35:50

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China itaendelea kutekeleza jukumu la kulinda usalama wa meli katika Ghuba ya Aden na eneo la bahari ya Somalia, kupanua ushirikiano wa kimataifa katika ulinzi wa meli, kutekeleza majukumu ya kulinda amani na utulivu wa kimataifa na kikanda, na kulinda usalama wa njia muhimu ya kimataifa.

    Hivi karibuni katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres alitoa ripoti kuhusu suala la uharamia la Somalia kwenye baraza la usalama, na ripoti hii imetaja mara kwa mara mchango wa China katika kulinda usalama wa meli kwenye eneo hilo. Bw. Geng Shuang amesema China inafurahishwa na katibu mkuu kwa kusifu mchango wa China katika ripoti yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako