• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuanza kuuza mafuta nje kuanzia Disemba mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-10-27 20:01:29

    Kenya inatarajiwa kuanza kuuza mafuta ghafi kwa kiwango kidogo kuanzia Disemba mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari, waziri wa nishati wa Kenya Bw Alfred Keter hatua hiyo inalenga kuona jinsi mafuta hayo ghafi ya Kenya yatakavyopokelewa katika soko la kimataifa. Amesema hivi sasa wanaendelea kujenga miundo mbinu itakayorahisisha usafirishaji wa mafuta hayo kwa wingi. Serikali ilikuwa imepanga kuanza kusafirisha mafuta hayo Juni mwaka huu lakini ikalazimika kuahirisha kutokana na maandalizi ya uchaguzi Agosti 8.Visima vya mafuta katika eneo la Turkana vinakisiwa kudumu kwa muda wa miaka 25.Bomba la kusafirisha mafuta linalojengwa hivi sasa linatarajiwa kusafirisha mapipa laki 1 kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako