• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dar es Salaam. Tanzania kuhakikisha bidhaa zake hazizuiliwi katika nchi za EAC

    (GMT+08:00) 2017-10-27 20:01:59

    Serikali ya Tanzania imesema haitakubali kuona bidhaa kutoka Tanzania zinazuiliwa kuingia katika nchi yoyote ya Afrika Mashariki kwa kuwa mkataba wa soko la Pamoja wa nchi hizo (EAC) unaruhusu kufanya biashara katika ukanda huo.

    Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda amesema hayo wakati wa mjadala wa pamoja kuhusu mchango wa kampuni za kati na ndogo katika kufikia nchi ya viwanda na ushirikishaji wa wazawa. Kabla ya mjadala huo, utafiti wa kampuni 100 za kati Tanzania uliwasilishwa kwa wadau na kubainisha changamoto mbalimbali ambazo kampuni hizo zinapitia katika ufanyaji wa biashara zao.

    Utafiti uliofanywa na kampuni ya Research Solutions Africa umebaini kwamba theluthi mbili ya kampuni 4,000 zilizoshindanishwa zilionyesha nia ya kupanua biashara zao mpaka nchi nyingine za Afrika Mashariki.

    Hata hivyo, zililalamikia upungufu wa mitaji ya kuziwezesha kupanua biashara zao. Pia, zimelalamikia utitiri wa kodi, jambo ambalo zilisema linaathiri mitaji yao na ufanyaji wa biashara nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako