• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dar es Salaam. Kampuni ya madini ya Barrick kuilipa serikali ya Tanzania dola milioni 300

    (GMT+08:00) 2017-10-27 20:02:38

    Licha ya kupata hasara kwenye robo ya tatu ya mwaka, kampuni ya Barrick imetenga dola 300 milioni za Marekani (zaidi ya Sh660 bilioni) kuilipa Serikali lakini imetaka iruhusiwe kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi.

    Acacia, ambayo ni kampuni tanzu ya Barrick na inayomiliki migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, ilikuwa imezuiwa tangu machi mwaka huu kusafirisha mchanga huo wa madini kwenda kuuyeyusha nje ya nchi kwa ajili ya kupata mabaki ya dhahabu, shaba, fedha na madini mengine yaliyoshindikana kuchenjuliwa migodini.

    Baada ya majadiliano baina ya Serikali na Barrick, kampuni hiyo ya Canada ilikubali kulipa dola 300 milioni kuonyesha uaminifu wake.

    Taarifa ya miezi mitatu ya Barrick inaonyesha kuwa ilipata hasara ya dola 11 milioni ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni 24 tofauti na faida ya zaidi ya shilingi bilioni 385 iliyopata katika kipindi kama hicho mwaka jana. Barrick inasema kupungua kwa mapato yake kumechangiwa na ongezeko la makadirio ya kodi yanayofika dola 172 milioni zilizopendekezwa kwenye majadiliano ya mustakabali wa operesheni za Acacia nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako