• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya Uchaguzi yasimamisha upigaji kura magharibi mwa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-10-28 18:22:25

    Tume ya Uchaguzi nchini Kenya jana imesimamisha marudio ya upigaji kura wa uchaguzi wa uraisi katika kaunti nne magharibi mwa Kenya ambazo zimeathirika na machafuko na maandamano tangu Alhamisi.

    Mwenyekiti wa tume huru na mipaka ya uchaguzi (IEBC) Wafula Chebukati amesema uchaguzi huo hapo awali uliahirishwa hadi Oktoba 18, umesimamishwa katika vituo 3,635 vya kupigia kura katika kaunti za Kisumu, Siaya, Homabay na Migori.

    Chebukati pia amesema baadhi ya wafanyakazi wa tume hiyo walitekwa, kuteswa katika baadhi ya maeneo na baadhi ya nyumba zao kuvunjwa na kuporwa, huku wengine wakizuiwa kufika kwenye vituo vya kupigia kura na kufukuzwa.

    Wakati huo, waangalizi wakuu saba wa kimataifa wametoa wito kwa wakenya kuwa watulivu baada ya kumaliza uchaguzi mpya wa urais ambao umegawa nchi hiyo.

    Waangalizi hao kutoka Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na mashirika mengine wamesisitiza wakenya kuepuka vitendo kinyume na sheria na kuheshimu utawala wa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako