• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Burundi washerehekea kujiondoa kutoka ICC

    (GMT+08:00) 2017-10-28 18:22:52

    Waziri wa haki wa Burundi Bibi Aimee Laurentine Kanyana amesema kujiondoa kwa nchi hiyo katika mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) ni ushindi kwa nchi hiyo.

    Jana Ijumaa, maafisa wakuu wa jeshi, na maofisa wa polisi walisheherekea nchi hiyo kujiondoa kwenye mahakama hiyo baada ya kutoa maombi kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

    Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alitia saini amri ya nchi hiyo kujitoa kwenye mkataba wa Roma unaosimamia mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) kujiondoa mwezi Oktoba mwaka 2016, kufuatia muswaada uliopitishwa Oktoba 12, mwaka 2016 na Bunge la nchi hiyo.

    Bibi Aimeer ameeleza kuwa, sababu ya Burundi kujiondoa kunatokana na mahakama hiyo imekuwa chombo dhidi ya nchi za kiafrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako