• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Uhispania yachukua mamlaka ya serikali ya eneo la Catalonia kwa pande zote

    (GMT+08:00) 2017-10-28 18:32:39

    Waziri mkuu wa Uhispania Bw. Mariano Rajoy jana usiku alitoa hotuba katika televisheni akitangaza kuondoa madaraka ya mwenyekiti wa eneo linalojitawala la Catalonia Bw. Carles Puigdmeont, kuvunja bunge la eneo hilo, na kutangaza kufanya uchaguzi wa eneo hilo tarehe 21 mwezi Desemba.

    Bw. Rajoy alitangaza hatua nyingine za lazima zikiwemo kuondoa madaraka ya maofisa wote wa serikali ya eneo la Catalonia, kuondoa madaraka ya mkuu wa polisi wa eneo hilo na kufunga ofisi zote za eneo hilo kwenye nchi za nje.

    Nchi na mashirika ya bara la Ulaya na bara la America zilitoa maoni ya kuiunga mkono serikali ya Uhispania kulinda umoja wa taifa. Umoja wa Ulaya haukubali matokeo ya upigaji kura wa Catalonia. Serikali ya Ujerumani iliiunga mkono Uhispania kurudisha utaratibu wa katiba na pia kuzisisitiza pande husika zifanye juhudi kutuliza hali ya wasiwasi na kutatua mgogoro kwa kupitia mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako