• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 25 wauawa kutokana na shambulio mjini Mogadishu

    (GMT+08:00) 2017-10-29 18:35:01

    Watu wasiopungua 25 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea jana kwenye gari nje ya hoteli maarufu ya Nasahablod 2 mjini Mogadishu, Somalia.

    Kwa mujibu wa polisi, watu 30 akiwemo afisa wa serikali waliokolewa kutoka hotelini hapo wakati mapigano yakiendelea kati ya kundi la Al-Shabaab na vikosi vya usalama.

    shambulio limekuja wiki mbili baada ya watu zaidi ya 350 kuuawa kwa bomu lililotegwa kwenye lori lililolipuka kwenye mtaa wenye pilika mjini Mogadishu, shambulio hilo likiwa ni baya zaidi katika historia ya mji mkuu huo wa Somalia huku serikali ya Somalia ikilaani Al-Shabaab kuhusika na tukio hilo.

    mashambulizi hayo yametokea wakati viongozi wa nchi wakiwasili Mogadishu kwa mkutano wa kiwango cha juu cha usalama ambao ulipangwa kuanza leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako