• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Joshua amdunda Takam kwa TKO raundi ya 10 na kutetea taji la IBF

  (GMT+08:00) 2017-10-30 08:51:17

  Anthony Joshua ameshinda kwa Technical Knockout (TKO) katika raundi ya 10 ya mpambano na kutetea taji lake la uzito wa juu (IBF) baada ya kumtwanga Carlos Takam, pambano lililopigwa kwenye ukumbi wa Principality mjini Cardiff, Uingereza.

  Refa alisimamisha mpambano huo na kumuokoa Takam aliyekuwa akitokwa na damu nyingi usoni kufuatia kuchanika juu ya jicho mwanzoni mwa pambano hilo.

  Takam alichukua nafasi hiyo ya kupigana na Joshua baada ya mpinzani aliyepangwa awali Kubrat Pulev kujitoa baada ya kuumiza mazoezini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako