• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Syria yasema mji wa Raqqa uko mikononi mwa kundi la IS licha baada ya kundi la IS kushindwa

    (GMT+08:00) 2017-10-30 09:02:13

    Wizara ya mambo ya nje ya Syria imesema mji wa Raqqa ambako hivi karibuni kundi la IS lilishindwa kwenye mapambano, bado unakaliwa na muungano unaoongozwa na Marekani na wapiganaji wa kundi la SDF.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema mji wa Raqqa bado ni mji unaokaliwa, na utaendelea kuchukuliwa kama ni mji unaokaliwa hadi jeshi la serikali ya Syria litakapoingia kwenye mji huo.

    Taarifa hiyo imesema Marekani na washirika wake wanafurahia kile wanachoita ukombozi wa mji wa Raqqa kwenye miili ya watu waliouawa huku asilimia 90 ya mji huo ikiwa imeharibiwa.

    Mji wa Raqqa ulikombolewa Oktoba 17 na jeshi la kidemokrasia la Syria SDF kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS. Mwaka 2014 kundi hilo liliutangaza mji wa Raqqa kuwa mji mkuu wa dola yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako