• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waethiopia 245 wakamatwa kutokana na kufanya ghasia

    (GMT+08:00) 2017-10-30 09:25:07

    Serikali ya jimbo la Oromia la Ethiopia imetangaza kuwakamata watu 245 wanaotuhumiwa kufanya ghasia katika jimbo hilo.

    Msemaji wa serikali ya jimbo hilo Bw Addisu Arega amesema, maandamano ya kimabavu yaliyotokea hivi karibuni yamesababisha vifo vya watu 11, gari moja kuchomwa na kuhujumu shughuli za kiuchumi za kawaida. Amesema watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na maandamano hayo na pia wanatuhumiwa kuchochea chuki kati ya makabila tofauti.

    Hali kwa sasa imedhibitiwa kutokana na juhudi za serikali kuu na serikali ya jimbo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako