• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia asema mashambulizi yanayoongezeka hayatazuia juhudi za kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-10-30 09:35:40

    Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia amesema mashambulizi ya kigaidi yaliyoongezeka nchini Somalia hayatazuia juhudi za nchi hiyo kupambana na ugaidi.

    Rais Mohamed anasema hayo siku moja baada ya kundi la Al-Shabaab kutangaza kuwajibika na mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 20 wakiwemo wabunge, maofisa wa usalama na viongozi wa kikanda katika hoteli ya Nasa Hablod II. Amesema wapiganaji hao wanajaribu kuzusha hofu miongoni mwa wasomali.

    Amesema kundi la Al-Shabaab lina hofu kwa kuwa wananchi wote wamedhamiria kushiriki katika mchakato wa kutafuta amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako