• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa msaada wa dharura wa chakula nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-10-30 18:52:56

    Hafla ya kukabidhi sehemu ya kwanza ya msaada wa dharura wa chakula uliotolewa na China kwa serikali ya Afghanistan ilifanyika jana huko Kabul. Kaimu balozi wa China nchini Afghanistan Bw. Zhang Zhixin na kaimu waziri wa usimamizi wa maafa ya taifa na mambo ya binadamu wa Afghanistan Bw. Mohammad Aslam Sayas walihudhuria hafla hiyo.

    Bw. Zhang Zhixin alisema China ilitangaza kutoa msaada wa chakula wenye thamani ya renminbi bilioni 2 kwa nchi zinazoendelea chini ya pendekezo la "Ukanda mmoja na njia moja", msaada huu ni hatua halisi ya kutekeleza ahadi hiyo. Aidha alisema China siku zote inaiunga mkono Afghanistan kufanya ukarabati wa amani, na msaada wake utasaidia raia wa Afghanistan kuboresha hali ya maisha na kutatua kihalisi matatizo.

    Habari nyingine zinasema, wapiganaji 12 waliuawa na wengine 12 kujeruhiwa katika mapambano kati ya kundi la Taliban na tawi la kundi la Islamic State IS kwenye mkoa wa Nangarhar. Miongoni mwa wapiganaji waliouawa, ni pamoja na kiongozi wa kundi la Taliban kwenye eneo la Dara-e-Noor, Sayyed Aga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako