• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapato ya Sekta ya Utamaduni ya China yakuwa zaidi katika robo tatu za mwanzo mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-10-30 18:54:37

    Kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa leo na Bodi ya Takwimu ya Taifa, mapato katika sekta ya utamaduni ya China yamekuwa zaidi katika robo tatu za mwanzo za mwaka huu.

    Sekta hii imeshuhudia mapato yake yakiongezeka na kuwa asilimia 11.4 na kufikia yuan trilioni 6.8 yakiwa yamekuwa zaidi kwa asilimia 4.4 kuliko mwaka jana wakati kama huu. Bodi imefuatilia karibu kampuni 54,000 kwenye sekta 10 za utamaduni, sita zikiwa za kutoa huduma na 4 za utengenezaji.

    Mapato ya huduma za utamaduni ya "Internet Plus" bado yamebaki kuwa imara, ambapo yale ya huduma za taarifa za utamaduni yakipanda kwa asilimia 36. Mkoa ulioendelea zaidi wa mashariki umechangia asilimia 75.1 ya mapato ya jumla, na ambao haujaendelea wa magharibi umeripotiwa kukua kwa kasi kuliko mikoa mingine, ukiwa na ongezeko la mapato la asilimia13.4. China inapanga kukuza sekta ya utamaduni na kuwa eneo muhimu la uchumi hadi kufikia mwaka 2020, kwa kuboresha miundo mbinu yake, kuhamasisha chapa kubwa na kuongeza matumizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako