• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maendeleo ya uchumi wa China kuhitaji ushirikiano zaidi wa kimataifa

  (GMT+08:00) 2017-10-30 18:59:33

  Mkutano wa mwaka wa uchumi wa China na ushirikiano wa kimataifa ambao pia ni mkutano mpya wa "Meli ya Bashan" ulifanyika hivi karibuni hapa Beijing. Wataalamu waliohudhuria mkutano huo wenye kauli mbiu ya "China baada ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikoumunisti cha China na dunia" wanaona kuwa uchumi wa China umeingia katika kipindi cha maendeleo bora, na utahitaji ushirikiano zaidi wa kimataifa.

  China imetoa ripoti kwenye mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, ikiamua kujenga muundo wa kisasa wa uchumi, na kudhihirisha kuwa uchumi wa China umeingia kwenye kipindi cha maendeleo bora kutoka kipindi cha maendeleo ya kasi, na ujenzi wa muundo wa kisasa wa uchumi, ni mahitaji ya haraka ya kupiga hatua muhimu, na lengo la kimkakati la maendeleo ya China. Profesa Su Jian wa chuo cha elimu ya uchumi cha Chuo Kikuu cha Beijing, anaona China inaweza kudumisha kasi ya maendeleo ya uchumi wakati inaboresha sifa ya uchumi wake. Anasema,

  "Katika kipindi cha miaka 30 kati ya mwaka 2020 na 2050, China itakuwa na kazi ngumu ya kuendeleza uchumi. Sasa tunajitahidi kupata maendeleo bora, ambayo hayakinzani na maendeleo ya kasi, na tutajaribu kupata maendeleo ya kasi yenye sifa nzuri."

  Wataalamu wengi waliohudhuria mkutano huo wanaona ujenzi wa muundo wa kisasa wa uchumi, hauwezi kukosa soko ambalo linafanya kazi kuu za kupanga maliasili, pamoja na serikali ambayo inafanya kazi za usimamizi na uvumbuzi. Naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Umma cha China Profesa Liu Yuanchun, ambaye pia ni mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo na Mikakati ya Taifa la China anaona kuwa, mkakati wa mageuzi ya China katika kipindi kipya umebadilika,

  "China inapaswa kusukuma mbele mageuzi katika mfumo wa fedha na kodi unaozingatia maslahi ya serikali za sehemu mbalimbali, mfumo wa ukaguzi unaozingatia vitendo vya serikali, mfumo wa kutoa maelezo ya sera, pamoja na mawazo ya jadi ya chama na serikali yetu."

  Mkutano mkuu wa 19 wa CPC pia umedhihirisha lengo kuu la mambo ya kidiplomasia ya China, ambalo ni kusukuma mbele ujenzi wa aina mpya ya uhusiano wa kimataifa na jumuiya yenye mustakabali wa pamoja. Profesa Jia Qingguo, ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya uhusiano wa kimataifa ya Chuo Kikuu cha Beijing anaona kuwa, China itahitaji zaidi ushirikiano wa kimataifa katika siku zijazo. Anasema,

  "Ushirikiano na mafanikio ya pamoja ndio lengo letu, na utawala wa kimataifa unapaswa kukabiliana na kutatua masuala na changamoto za kimataifa, ikiwemo biashara, uwekezaji, uhalifu wa kuvuka mipaka, wahamiaji haramu, ugaidi, mazingira, usalama wa mtandao wa internet, silaha za maangamizi na nyinginezo. China itahitaji zaidi ushirikiano wa kimataifa siku hadi siku."

  Wataalamu waliohudhuria mkutano huo pia wanaona kuwa, China itaendelea kufuata njia ya kujiendeleza kwa amani, kuongeza maslahi ya pamoja na nchi nyingine, na kutetea uratibu na ushirikiano kati ya nchi kubwa. Kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani, Profesa Zhang Shengjun wa Chuo Kikuu cha Umma cha China, ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa utawala wa kimataifa cha China, anaona China na Marekani zitafanya ushirikiano zaidi katika siku zijazo.

  "Mkutano mkuu wa 19 wa CPC umeondoa wasiwasi wa China na dunia. Hali ya sasa imethibitisha China itaendelea kwa utulivu. Naona katika siku za baadaye, China na Marekani zitakuwa na ushirikiano zaidi, kwani China haitaki kuchukua nafasi ya Marekani duniani, na nchi hizo mbili zina uhusiano zaidi wa kushirikiana kuliko kugongana."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako