• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuunga mkono umoja wa Hispania baada ya Catalonia kujitangazia uhuru

    (GMT+08:00) 2017-10-30 19:06:40

    China imesema inaunga mkono juhudi za serikali ya Hispania kuimarisha umoja wa kitaifa na ukamilifu wa ardhi baada ya bunge la Catalonia kujitangazia uhuru siku ya Ijumaa.

    Muda mfupi baada ya bunge kutoa tangazo lake, Waziri mkuu wa Hispania Mariano Rajoy alimfukuza kazi kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont na serikali yake na kutangaza uchaguzi mpya wa jimbo hilo utafanyika Disemba 21. Bunge la Hispania limepitisha hoja ya kifungu cha 155 cha katiba ya Hispania, ambacho kinasitisha madaraka ya Catalonia na kukabidhi taasisi muhimu kwa serikali kuu.

    Akiongea na wanahabari kuhusiana na hilo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema Msimamo wa China ni thabiti na uko wazi, na kwamba inaona ni mambo ya ndani ya Hispania. Aidha China inapinga mgawanyiko wa nchi na kukiuka utawala wa sheria na kuamini kuwa Hispania inaweza kulinda utaratibu wa jamii na haki za raia ndani ya sheria na mfumo wa kitaasisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako