• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio ya uporaji wa watalii wa kigeni yatokea nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2017-10-30 19:28:57

    Polisi nchini Afrika Kusini imethibitisha kuwa mwanamitindo maarufu wa Uingereza Bibi Sarah MacDonnell na wengine watano wameporwa huko Cape Town, ila hakuna mtu aliyejeruhiwa. Hii ni mara ya pili kwa watalii wa kigeni kuporwa katika wiki iliyopita huko Cape Town.

    Mapema wiki hii, wanandoa kutoka Singapore nao pia waliporwa mali zaona majambazi kadhaa wakiwa garini eneo la Mitchell, na kumpiga mwanamume mmoja.

    Mbali na Cape Town, matukio ya uporaji wa watalii wa kigeni pia yaliyotokea katika sehemu nyingine nchini humo. Majambazi wenye silaha walivamia hoteli moja huko Limpopo na kuwapora wateja wote wa hoteli hiyo.

    Hivi karibuni, hali ya usalama ya Afrika Kusini inazidi kuwa mbaya. Takwimu zilizotolewa na wizara ya polisi ya nchi hiyo zimeonesha kuwa tangu mwezi Aprili mwaka jana hadi Machi mwaka huu, idadi ya uhalifu mbaya kurekodiwa imefikia milioni 2.1, ambapo kesi za mauaji ziliongezeka kwa asilimia 1.8 huku uporaji ukiongezeka kwa asilimia 6.4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako