• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Korea Kusini kutimiza ahadi yake na kushughulikia vizuri suala husika

    (GMT+08:00) 2017-10-30 19:29:15

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesisitiza kuwa China inaitaka Korea Kusini kutekeleza ahadi yake na kushughulikia vizuri suala la mfumo wa kukinga makombora wa Thaad , ili kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili kurudi katika hali ya utulivu.

    Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumzia hoja ya waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini Bibi Kang Kyung-wha kuhusu suala la mfumo wa kukinga makombora wa Thaad. Bibi Kang alipohojiwa na bunge la Korea Kusini alisema, msimamo wa serikali ya nchi hiyo wa kutojiunga na mfumo wa kukinga makombora wa Marekani hautabadilika, ushirikiano wa usalama kati ya Korea Kusini, Marekani na Japani hautaendelezwa kuwa muugano wa kijeshi wa pande tatu. Aidha, serikali ya nchi hiyo haitafikiria kuzidisha mfumo wa Thaad.

    Bibi Hua amesema, China inatalia maanani katika msimamo wa Korea Kusini na siku zote inapinga Marekani kuweka mfumo wa Thaad nchini humo. China inaitaka Korea Kusini kutekeleza ahadi iliyoitowa na kuhimiza kurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili uwe wa hali ya kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako