Kampuni ya nishati ya nyuklia ya Russia Rosatom imesema Russia na Nigeria zimesaini makubaliano kuhusu ujenzi na uendeshaji wa kituo cha umeme wa nyuklia na kituo cha utafiti nchini Nigeria. Makubaliano hayo yalisainiwa kwenye mkutano wa mawaziri kuhusu matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia uliofanyika Abu Dhabi. Naibu mkuu wa idara ya masoko na maendeleo ya kibiashara ya kampuni ya Rusatom Anton Moskvin amesema miradi hiyo itahimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na maendeleo ya teknolojia ya nyuklia yataiwezesha Nigeria kuimarisha hadhi yake ya uongozi barani Afrika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |