• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNHCR yahimiza mashirika ya kimataifa kufuatilia zaidi suala la wakimbizi nchini DRC

    (GMT+08:00) 2017-10-31 08:54:56

    Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limehimiza mashirika ya kimataifa kufuatilia zaidi msukosuko wa wakimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC unaozidi kuwa mbaya.

    Mwakilishi wa UNHCR nchini Zambia Bibi Pierrine Aylara ameshukuru jitihada zinazofanywa na serikali ya Zambia na pande nyingine zilizotoa mchango. Amesema, nchi kama Zambia zinahitaji misaada ya dharura ili kukabiliana na ongezeko la idadi ya wakimbizi.

    Kamishna wa wizara ya mambo ya ndani ya Zambia anayeshughulikia masuala ya wakimbizi Bw Abdon Mawere, amesema hivi sasa kituo cha mpito kinapokea wakimbizi 50 hadi 100 kila siku. Wakimbizi 5,890 wamepata makazi, asilimia 60 kati yao wakiwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako