• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya kimataifa yakutana Sudan kuhimiza mazungumzo ya ndani ya Darfur

    (GMT+08:00) 2017-10-31 08:55:33

    Mkutano wa Mazungumzo ya ndani ya Darfur umefanyika jana mjini Khartoum, Sudan.

    Wajumbe kutoka jumuiya za Darfur, serikali ya Sudan, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Tume ya pamoja ya Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur UNAMID wameshiriki kwenye mkutano huo.

    Makamu wa rais wa Sudan Bw Hassabo Mohamed Abdul-Rahman alihutubia ufunguzi wa mkutano huo, akisema hali ya eneo la Darfur imepata maendeleo kutokana na makubaliano ya Doha kuhusu amani katika jimbo la Darfur (DDPD). Amesisitiza umuhimu wa kuendeleza mazungumzo hayo kati ya pande zote za eneo hilo ili kusimamisha mapambano.

    Wakati huo huo, mjumbe maalumu wa UNAMID Bw Jeremiah Mamabolo ameyahimiza makundi ambayo hayajasaini makubaliano hayo wajiunge na mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako