• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaendelea kutoa misaada kwa Syria inayokumbwa na vita

    (GMT+08:00) 2017-10-31 11:57:53

    Balozi wa China nchini Syria Bw. Qi Qianjin amesema China itaendelea kutoa misaada kwa Syria inayokumbwa na vita. Balozi Qi amesema hayo alipofanya ukaguzi katika mashirika yaliyoko mjini Manin, kaskazini mwa Damascus, yanayopokea misaada kutoka China kupitia Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu ICRC, kwa kushirikiana na Shirika la Hilali Nyekundu nchini Syria SARC.

    Bw. Qi amesema mwezi Mei serikali ya China ilichangia dola za kimarekani milioni 1 kwa ICRC kwa ajili ya operesheni za utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, ikiwa ni pamoja na maji safi, chakula, makazi ya muda na dawa kwa ajili wakimbizi wa ndani na wahamiaji kutoka nchi za jirani .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako