• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenyatta atangazwa mshindi katika uchaguzi mpya wa urais nchini Kenya

  (GMT+08:00) 2017-10-31 09:45:06

  Rais Uhuru Kenyatta ametangazwa mshindi katika marudio ya uchaguzi mpya wa urais uliofanyika tarehe 26 Oktoba nchini Kenya.

  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) Bw Wafula Chebukati, amemtangaza Bw Kenyatta kuwa mshindi baada ya kupata kura milioni 7.48 ambazo ni sawa na asilimia 98.27 ya kura zote zilizopigwa, katika uchaguzi ambao mshindani mkuu Raila Odinga alijiondoa.

  Bw. Chebukati alisema masharti yote yaliyowekwa kwa ajili ya uchaguzi mpya wa urais yalitimizwa, na kuhakikisha kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki. Pia amesema hatua zote zilifuatwa kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika vizuri, na kushughulikia dosari zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu uliopita wa tarehe 8 Agosti, uliofutwa na mahakama kuu ya Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako