• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapata ufanisi dhahiri katika kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa uchafuzi

    (GMT+08:00) 2017-10-31 17:44:57

    Serikali ya China leo hapa Beijing imetoa ripoti ya mwaka 2017 kuhusu sera na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, ikionesha kuwa kutokana na juhudi mfululizo, matumizi ya makaa ya mawe nchini China yanapungua, na uwezo wa kuzalisha umeme kwa nishati za maji, upepo na jua, na ukubwa wa viwanda vinavyojengwa vya kuzalisha umeme kwa nishati ya nyukilia unachukua nafasi ya kwanza duniani. Ripoti hiyo imesema China inatarajia kutimiza lengo la mwaka 2020 la kudhibiti kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyopangwa utoaji wa hewa inayoweza kuongeza joto duniani, na kuweka msingi mzuri kwa ajili ya kutimiza lengo la mwaka 2030.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ya Kamati ya Mageuzi ya China Bw. Li Gao amesema, katika miaka ya hivi karibuni, China imesukuma mbele kwa nguvu kubwa juhudi za kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa uchafuzi, kwa kudhibiti matumizi ya makaa ya mawe, kupiga marufuku ongezeko la uzalishaji wa makaa ya mawe, na kuharakisha kufuta uzalishaji ulioko nyuma kimaendeleo.

    "Tangu mpango wa 13 wa miaka mitano uanze kutekelezwa , matumizi ya makaa ya mawe katika nishati zote yanakadiriwa kupungua kwa zaidi ya asilimia tatu. Katika robo tatu zilizopita mwaka huu, uzalishaji wa makaa ya mawe wa mashirika makubwa umepungua kwa asilimia 10.6 ukilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Kwa mujibu wa makadirio ya Shirikisho la Viwanda vya Makaa ya Mawe la China, katika robo tatu zilizopita mwaka huu, China imetumia makaa ya mawe tani bilioni 2.84, na kupungua kwa asilimia 2.4 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, huku uzalishaji wa umeme kwa nishati za maji, nyukilia na upepo ukiongezeka kwa asilimia21.1."

    Ripoti hiyo inaonesha kuwa mwaka 2016 utoaji wa carbondioxide nchini China ulipungua kwa asilimia 6.6, na umeendelea kupungua kwa asilimia 4 katika robo tatu zilizopita mwaka huu.

    Mjumbe maalumu wa China kwenye suala la mabadiliko ya hali ya hewa Bw. Xie Zhenhua amesema, katika miaka 10 iliyopita, China imepunguza utoaji wa carbondioxide kwa tani bilioni 4.1 wakati inadumisha maendeleo ya kasi ya uchumi, na kufanikiwa kutimiza uwiano wa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuendeleza uchumi na jamii. Anasema,

    "China imechagua njia ya kujiendeleza ambayo inazingatia uhifadhi wa mazingira na kupunguza utoaji wa carbondioxide. Hivi sasa uchumi wetu unaendelea vizuri na kwa utulivu, huku tukitekeleza vizuri hatua za kupunguza utoaji wa hewa inayoweza kuongeza joto duniani."

    Mkutano wa 23 wa nchi zilizosaini makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa utafanyika kuanzia tarehe 6 hadi 17 mwezi Novemba huko Bonn, Ujerumani. Mkutano huo utafanya mazungumzo zaidi kuhusu Makubaliano ya Paris, ili kutunga mpango wa kutekeleza majukumu mbalimbali yaliyowekwa kwenye makubaliano hayo. Bw. Xie anasema,

    "China itatoa mpango wake katika mkutano huo. Hivi sasa tuna mivutano mbalimbali. Mpango wa China unaitwa "mpango wa kuunda madaraja", na China inatumai pande zinazohusika zitakuwa karibu na kufanya juhudi za pamoja, ili hatimaye kupata njia ya kutatua mivutano hiyo."

    Bw. Xie pia amesema kuwa majukumu ya kukabiliana na suala la mabadiliko ya hali ya hewa ni ya haraka, yanahitaji nchi zote kuchukua hatua halisi, na kufikia makubaliano mapema kuhusu mpango wa kutekeleza Makubaliano ya Paris, ambayo yataelekeza juhudi zao za kukabiliana na suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako