• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa laitisha mkutano kujadili uungaji mkono wa kikosi cha pamoja cha eneo la Sahel

    (GMT+08:00) 2017-10-31 18:43:41

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeitisha mkutano wa ngazi ya mawaziri kujadili njia zinazoweza kutumiwa na jumuiya ya kimataifa kuliunga mkono kundi la nchi za Sahel kuanzisha kikosi cha pamoja kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw Antonio Guterres amesema uungaji mkono wa kisiasa wenye nguvu, pamoja na wa mali na kiutendaji, ni muhimu katika kuzisaidia nchi hizo kupambana na changamoto ya ugaidi.

    Kundi la nchi tano za Sahel G5 linahusisha Mali, Mauritania, Burkina Faso, Niger na Chad, ambako mara kwa mara walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa na raia wamekuwa wakishambuliwa na wanamgambo wa kiisalamu.

    Bw. Guterres amesema umasikini, kukosa maendeleo na mabadiliko ya hali ya hewa vimefanya changamoto zinazolikabili eneo hilo kuwa kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako