• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China inafikiria kuwachukulia adhabu wanaodharau wimbo wa taifa

    (GMT+08:00) 2017-10-31 18:44:05

    Bunge la China linafikiria kufanya marekebisho ya sheria ya makosa ya jinai na kuweka adhabu kwa kosa la kutoheshimu wimbo wa taifa.

    Rasimu ya marekebisho hayo imewasilishwa kujadiliwa kwenye kamati ya kudumu, ya bunge la umma la China. Kwa mujibu wa rasimu hiyo, watu watakaokutwa na kosa la kutoheshimu wimbo wa taifa wanaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka mitatu.

    Rasimu hiyo pia inasema wale watakaobadilisha maneno ya wimbo, au kupiga na kuimba wimbo wa taifa kwa njia isiyo na adabu watawekwa kizuizini kwa muda wa siku 15, au kushitakiwa kwa kosa la jinai. Rasimu pia inasema sheria ya kutoheshimu wimbo wa taifa pia itawahusu watakaofanya makosa yanayohusiana na bendera ya taifa na nembo ya taifa

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako