• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia aahidi kuharakisha kazi ya uratibu wa vikosi vya usalama

    (GMT+08:00) 2017-10-31 18:44:31

    Rais Mohamed Abdulahi Farmajo wa Somalia amesema kuwa serikali yake itaharakisha kazi ya kuratibu vikosi vya usalama vya serikali kuu na serikali za majimbo, ili kupambana kwa pamoja na kundi la Al Shabaab.

    Akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano uliowakutanisha wakuu wa usalama wa majimbo, Rais Farmajo amesema Somalia inahitaji mkakati wa pamoja kulishinda kundi la Al Shabaab, ambalo katikati ya mwezi huu lilifanya mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu 350.

    Amesema baada ya mkutano huo wanatarajia kuwa maofisa hao wataweka mpango na kuunganisha vikosi vya usalama vya majimbo na serikali kuu, ili kulishinda na kulitokomeza kundi la Al Shabaab. Pia ameomba uungaji mkono zaidi kutoka kwa vikosi vya nchi jirani zinazochangia askari kwenye jeshi la tume ya Umoja wa Afrika, kuimarisha operesheni zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako