• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kujiunga tena na makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2017-10-31 19:13:17

    Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia suala la mabadiliko ya hali ya hewa Bw. Xie Zhenhua amesema, China inaitaka Marekani kujiunga tena na makubaliano ya Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, na kuchangia ajenda hiyo ya kimataifa kuhusu mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Bw. Xie amesema, China inataka kuanzisha ushirikiano na Marekani katika mazungumzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, baada ya nchi hiyo kusema itaendelea kuwepo katika mazungumzo hayo, ingawa imejitoa kutoka makubaliano hayo.

    Pia amesema, China imeweka bayana kwamba inapenda kuimarisha ushirikiano na Marekani katika maeneo ya matumizi ya nishati safi, hifadhi ya nishati na maliasili, kuhifadhi kaboni na utafiti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako