• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya Kimataifa yasisitiza kuendeleza nishati ya nyuklia kwa njia endelevu na salama

    (GMT+08:00) 2017-10-31 19:13:54

    Mkutano wa kimataifa wa awamu ya nne wa ngazi ya mawaziri kuhusu nishati ya nyuklia umefunguliwa huko Abu Dhabi, huku pande mbalimbali zikisisitiza kuhimiza nishati ya nyuklia kuendelezwa kwa njia endelevu na salama.

    Maofisa na wataalamu 700 kutoka nchi na sehemu 67 wanahudhuria mkutano huo wa siku tatu, ambao utajadili mchango mkubwa uliotolewa na nishati ya nyuklia katika kuhimiza maendeleo, kutatua uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa, na kutafiti mwelekeo na changamoto zinazoikabili nishati hiyo.

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Kimataifa Bw. Yukiya Amano ametoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano huo akisema, katika miongo kadhaa ijayo, nishati ya kinyuklia itatoa mchango mkubwa katika maendeleo endelevu ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako