• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Huenda Canada na Australia zikanunua madini ya Coltan kutoka Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-10-31 19:42:53

    Makampuni ya madini ya Canada na Australia yanapanga kuanza kununua madini aina ya Coltan kutoka Rwanda ambako wanaweza kuyapata kwa bei nafuu.

    Rwanda sio mzalishaji mkuu wa madini hayo lakini kiasi cha asilimia 90 ya Coltan nchini humo kinaweza kuingia kwenye soko la kimataifa.

    Mkurungezi wa madini, gesi na petrol Francis Gatare hajatoa taarifa zaidi lakini amesema baadhi ya makampuni ya nchi hizo mbili wamezuru Rwanda kutathmini uwezekano wa kuagiza madini hayo.

    Coltan ni madini yanayohimili joto la juu na hutumika katika utengenezaji wa simu, magari ya umeme na bidhaa nyingine za ki elektroniki.

    Australia, Brazil, na Canada huzalisha asilimi 80 ya Coltan lakini sasa madini yao hayo yameendela kupungua ndani ya miaka 10 iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako