Kampuni ya kimataifa ya kilimo James Finlays nchini Kenya imepata hasara ya milioni 6 kutokana na mgomo wa wafanyakazi na uharibifu wa mali.
Kampuni hiyo imesema watu wasiojulikana walivamia na kuharibu mali.
Maneja wa kampuni hiyo Sammy Kurui, amesema uvamizi huo kwenye shamba la chai la Kaproret kaunti ya Bomet ni mojawepo wa uhalifu unatokea mara kwa mara dhidi ya kampuni hiyo.
Msemaji wa wafayakazi 15,000 wa Finlays Dickson Sang amesema uvamizi huo haukutekelezwa na wafanyakazi.
Wafanyakazi hao ni sehemu ya wenzao 40,000 ambao wanashinikiza kuongezwa mshahara kwa mujibu wa makubaliano ya mwaka 2015/16 kwa asilimia 30.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |