• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bandari ya Tanzania (TPA) kufungua ofisi zake nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-10-31 19:43:31

    Uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), umetekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufungua ofisi zake nchini Rwanda kwa lengo la kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa nchi hiyo.

    TPA imeshakamilisha taratibu zote na tayari ina ofisi na mtumishi wake nchini humo, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni ufunguzi rasmi wa ofisi hiyo jijini Kigali.

    Aidha, imeelezwa kuwa kumekuwa na ongezeko la shehena ya mizigo ya Rwanda kwa wastani wa asilimia 9.9 kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano, kutoka tani 630,000 mwaka 2012/2013 mpaka tani 950,000 mwaka 2016/2017.

    Haya yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko hivi karibuni alipokutana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura aliyeitembelea mamlaka hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako