• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Yusuf Manji kwenye mazungumzo kununua Nakumatt Tanzania.

    (GMT+08:00) 2017-10-31 19:43:47

    Mfanyabiashara tajiri wa Tanzania Yusuf Manji ametajwa kama mmoja wa watu wnaaopania kununua maduka ya Nakumatt Tanzania.

    Nakumatt Tanzania inadaiwa karibu dola milioni 380 na watu walioiuzia bidhaa na imekuwa ikifunga matawi yake mengi Afrika Mashariki kutokana na madeni.

    Yusuf Manji yuko kwenye mazungumzo na Nakumatt na anatarajia watafikia makubaliano.

    Wakati huo huo Nakumatt imefunga tawi lake la mjini Kisumu magharibi mwa Kenya.

    Tawi hilo lilifunguliwa miaka 19 iliopita na limekuwa likihudumu masaa 24.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako