Data zilizotolewa na ofisi ya takwimu ya Uingereza ONS zinaonesha kuwa uanachama wa Umoja wa Ulaya unamgharimu kila raia wa Uingereza wastani wa dola 163 za kimarekani kila mwaka. Data hizo zinasema dola bilioni 5.8 zaidi zilirudishwa kwenye sekta za umma na zile za binafsi za Uingereza kwa mwaka jana, na kuufanya mchango halisi wa Uingereza kwa Umoja wa Ulaya mwaka jana kufikia dola bilioni 12.5 za kimarekani, ikiwa ni nusu ya mchango wa jumla Uingereza iliotoa kwa Umoja huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |