• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yatoa mwito wa kufanyika kwa mazungumzo baada ya uchaguzi wa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-01 09:09:40

    Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika na shirika la maendeleo la kiserikali la nchi za Afrika mashariki IGAD, wamesema uchaguzi wa rais wa Kenya uliofanyika wiki iliyopita ulikuwa wa kuaminika, lakini wametaka pande zote za kisiasa kufanya mazungumzo ili kuondoa tofauti zao.

    Mkuu wa timu ya waangalizi ya Umoja wa Afrika Bw Thabo Mbeki amesema mchakato wa kufungua vituo vya kupigia kura, kupiga kura, kufungwa na kuheshabu kura ulienda vizuri, licha ya baadhi ya watu katika ngome ya upinzani kususia kura, kuandamana na kupinga idadi ya wapiga kura. Waangalizi wa IGAD wamesema uchaguzi uliendelea vizuri katika sehemu nyingi licha idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura kuwa ndogo.

    Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wametoa mwito kwa viongozi wa pande mbalimbali kufanya mazungumzo na kuondoa tofauti za kisiasa kwa njia ya kuwajibika.

    Wakati jumuiya hizo zikitoa mwito wa kutatuliwa kwa mvutano kwa njia ya mazungumzo kiongozi wa muungano wa NASA, Bw Raila Odinga amesema hatambui ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako