• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa ulinzi wa Uingereza atajwa kwenye kashfa ya ngono inayoendelea kulitikisa bunge la Uingereza

    (GMT+08:00) 2017-11-01 09:10:20

    Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Sir Michael Fallon amekuwa ni mwanasiasa wa hivi karibuni kutajwa kuhusika na kashfa ya ngono inayolitikisa bunge la Uingereza, baada ya wabunge wanawake wa bunge hilo kulalamika kuwa baadhi ya wabunge na mawaziri wamekuwa ni wadhalilishaji wa kijinsia.

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May ametoa mwito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka baada ya kutolewa kwa malalamiko hayo. Baadhi ya matukio yanatajwa kutokea zaidi ya miaka saba iliyopita.

    Waziri wa biashara ya kimataifa wa Uingereza Bw Mark Garnier tayari anafanyiwa uchunguzi kuhusiana na kashfa hiyo, kutokana na kumwagiza katibu muhtasi wake kwenda kumnunulia vifaa vya kutumiwa kwenye ngono.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako