• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa China na Russia wakutana

    (GMT+08:00) 2017-11-01 09:30:26
    Mawaziri wakuu wa China na Russia wakutana

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amekutana na mwenzake wa Russia Bw. Dmitry Medvedev ambaye yuko ziarani nchini China kuhudhuria Mkutano wa 22 wa mazungumzo ya mawaziri wakuu wa China na Russia.

    Mawaziri wakuu hao wamesifu maendeleo yaliyopatikana katika uhusiano kati ya pande hizo mbili. Bw. Li Keqiang amesema, Bw. Medvedev ni kiongozi wa kwanza wa kigeni kuitembelea China baada ya Mkutano mkuu wa 19 wa chama, hali inayoonesha ukaribu na kiwango cha juu cha uhusiano kati ya nchi mbili. Amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili, na kulinda kwa pamoja amani na utulivu, maendeleo ya ustawi wa dunia.

    Kwa upande wake Bw. Medvedev amepongeza kufungwa kwa mafanikio kwa Mkutano mkuu wa 19 wa chama, akieleza kuwa Russia inapenda kushirikiana na China kuhimiza uhusiano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako