Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa likisisitiza umuhimu wa kulinda haki na maslahi ya watoto kwenye migogoro ya kijeshi.
Taarifa hiyo inazihimiza pande mbalimbali za migogoro ziheshimu kazi ya mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na washirika wao, na kuwaruhusu watoe misaada kwa watoto kwa usalama, kwa wakati na bila vizuizi.
Taarifa inasema Baraza la usalama linalaani vitendo vya kuwatumikisha watoto jeshini, kuua, kubaka na kuteka nyara watoto, na kushambulia shule na hospitali, na kuzitaka pande zote zinazopambana zisitishe mara moja vitendo hivyo na kuchukua hatua maalum kulinda usalama wa watoto.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |