• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utekelezaji wa makubaliano ya Paris wahitaji pande zote kuharakisha hatua ya kupunguza utoaji wa carbondioxide

    (GMT+08:00) 2017-11-01 18:34:09

    Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa jana lilitoa ripoti likisema kuwa, hivi sasa ahadi ya kupunguza utoaji wa hewa zinazoongeza joto duniani iliyotolewa na nchi mbalimbali inaweza kufikia thuluthi moja ya lengo la kudhibiti hali ya hewa la mwaka 2030, na kwamba inahitaji pande zote zikiwemo sekta binafsi na serikali za mitaa kuongeza nguvu ili kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano ya Paris.

    Kutokana na makuabaliano hayo, pande zote zinakabiliana kwa pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa kwa njia zao zenyewe, ili kudhibiti kiwango cha wastani wa ongezeko la joto duniani ndani ya nyuzi 2 kuliko kipindi cha kabla ya viwanda, na kufanya juhudi ili kujaribu kudhibiti ongezeko hilo ndani ya nyuzi 1.5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako