• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yaitaka Kenya kufanya mazungumzo baada ya marudio ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2017-11-01 18:43:09

    Kufuatia kambi ya upinzani kukataa tena matokeo ya uchaguzi wa rais wa marudio uliofanyika tarehe 26 Oktoba, baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza rasmi Uhuru Kenyatta kuwa rais wa nchi hiyo, jumuiya ya kimataifa imezitaka pande za kisiasa kuendeleza umoja wa kitaifa na kufanya mazungumzo.

    Mwangalizi mkuu wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya Marietje Schaake amesema pande zinazopingana zimeiweka Kenya kwenye nafasi ngumu. Nao waangalizi wa uchaguzi wa shirika la maendeleo la kiserikali la nchi za Afrika Mashariki IGAD, wameitaka Kenya kuleta umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi wa marudio kuwagawa wananchi.

    Zaidi ya hayo msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema China inatumai pande husika za Kenya zitatatua tofauti zao kwa ufanisi na kuhakikisha amani na utulivu wa taifa baada ya uchaguzi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako