• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nchi zaidi ya 100 kuhudhuria kongamano la kimataifa la mwaka 2017 kuhusu ushirikiano wa uzalishaji

  (GMT+08:00) 2017-11-01 18:50:48

  Kongamano la kimataifa la mwaka 2017 kuhusu ushirikiano wa uzalishaji, ambalo pia ni mazungumzo ya 9 ya uwekezaji wa China katika nchi za nje litafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 22 hapa Beijing, na linatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe wa nyanja za siasa, mashirika, na taasisi za elimu na utafiti kutoka nchi na sehemu zaidi ya 100, ili kuhimiza ushirikiano wa uzalishaji duniani na ujenzi wa "ukanda mmoja, na njia moja".

  Kauli mbiu ya mazungumzo ya 9 ya uwekezaji wa China katika nchi za nje ni kukuza ushirikiano wa uzalishaji duniani, na kusukuma mbele ujenzi wa "ukanda mmoja, na njia moja". Kwenye mazungumzo hayo, viongozi wa nchi kadhaa na wakuu wa mashirika yanayohusika ya kimataifa watatoa hotuba, na wanaviwanda, wataalamu, wasomi mashuhuri na wajumbe wa mashirika makubwa watazungumzia uwekezaji katika nchi za nje, kuvutia uwekezaji kutoka nchi za nje, na ushirikiano wa uzalishaji duniani, ili kuchangia maendeleo ya uchumi wa dunia.

  Katibu mkuu wa Shirikisho la Maendeleo ya Shughuli za China katika Nchi za Nje lililoandaa mazungumzo hayo Bw. He Zhenwei, amesema licha ya kujenga vizuri zaidi jukwaa la kutangaza sera, kupashana habari na kutafuta uwekezaji, mazungumzo ya mwaka huu yataifahamisha dunia mpango mpya wa maendeleo ya China. Anasema,

  "Katika kipindi kati ya mwezi Januari na Septemba mwaka huu, uwekezaji wa China katika nchi za nje ulipungua kwa asilimia 41.9. Chanzo cha hali hii kitaelezwa na mkuu wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China kwenye mazungumzo hayo. Ataiondoa wasiwasi dunia kwa kufafanua kuwa sera ya China kuhusu uwekezaji katika nchi za nje haibadiliki. Mazungumzo ya mwaka huu yatafanyika baada ya mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China, hivyo pia tunataka kujulisha ripoti ya mkutano huo, ili watu wanaofuatilia China duniani waelewe zaidi mpango wa maendeleo ya China katika siku zijazo."

  Ili kuhimiza ushirikiano wa uzalishaji duniani, kongamano maalumu kuhusu ushirikiano wa kimataifa wa Shirikisho la Mambo ya Fedha ya Mtandao wa Mauzo wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" litafanyika wakati wa mazungumzo hayo. Naibu mwenyekiti wa shirikisho hilo Bi Wang Hui anasema,

  "Habari ya kwanza ni kuwa tutaanzisha taasisi ya utafiti na chuo cha biashara cha Shirikisho la Mambo ya Fedha ya Mtandao wa Mauzo wa 'Ukanda Mmoja na Njia Moja', kwa madhumuni ya kuitika wito wa baraza la serikali ya China kuendeleza mashirika 100 ya kimataifa yenye nguvu zaidi ya mtandao wa mauzo, kuanzisha mpango wa mashirika 1,000 kwa mtandao wa mauzo wa pendekezo la 'ukanda mmoja na njia moja', na kufundisha watu hodari 1,000 wa mambo ya fedha kwa mtandao huo."

  Habari zinasema mazungumzo ya 9 ya uwekezaji wa China katika nchi za nje yanayohusu sekta za miundombinu, utengenezaji wa mitambo, kilimo, biashara ya mtandao wa internet, uchukuzi wa bidhaa, reli, magari, safari za ndege, upashanaji habari, nishati mpya na nyinginezo, yatahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi na sehemu zaidi ya 100 duniani, zikiwemo Russia, Saudi Arabia, Australia na Kazakhstan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako