• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya inaongoza uchumi wa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara kwa kuandikisha rekodi mpya

    (GMT+08:00) 2017-11-01 19:27:15

    Kulingana na Ripoti mpya ya Benki ya Dunia ,Kenya inaongoza nchi nyengine za Kusini mwa jangwa la Sahara katika kuandikisha marekebisho kadhaa ya kibiashara kwa mwaka wa pili mfululizo.

    Toleo la maadhimisho ya miaka 15 ya Ripoti ya Kufanya Biashara ya Kundi la Benki ya Dunia, iliyotolewa jana, inaonyesha kwamba Kenya imetekeleza marekebisho mengi - sita kwa jumla - katika kanda ,mwaka uliopita.

    Miongoni mwa maboresho mengine,Kenya ilifanya uanzishaji wa biashara kuwa rahisi kwa kupunguza idadi ya taratibu zinazohitajika kuandikisha biashara kwa kutumia mfumo wa dirisha moja.

    Katika cheo cha Kimataifa,kwa urahisi wa Kufanya biashara,Mauritius inashikilia nafasi ya 25duniani,ikifuatiwa na Rwanda (41),na Kenya (80) ,nchi iliyoshikilia nafasi ya juu katika ukanda wa nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara.

    Kenya pia iliboresha upatikanaji wa umeme kwa kuwekeza katika nyaya za usamabazaji na transifoma na kuweka timu maalum inayoshughulikia na kurejesha umeme wakati unapokatika.

    Pia ilianzisha jukwaa la kwenye mtandao la kulipa kodi ya mpato..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako