• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yafanya vyema duniani katika Ripoti ya Benki ya Dunia ya ufanyaji biashara

    (GMT+08:00) 2017-11-01 19:27:32

    Utekelezaji wa marekebisho matano yameifanya Rwanda kupanda nafasi 15 katika Ripoti ya Benki ya Dunia ya ufanyaji biashara hadi na fasi ya 14 duniani.

    Rwanda ni ya pili katika bara la Afrika nyuma ya Mauritius katika Ripoti mpya iliyotolewa jana.

    Ripoti hiyo inaangalia kanuni na mazingira ambayo yanaboresha au kukwamisha ufanyaji biashara.

    Mwaka uliopita Rwanda ilishikilia nafasi ya 56 duniani.

    Kenya imeshika nafasi ya tatu Afrika na 80 duniani ikifuatiwa na Botswana iliyoshika nafasi ya 81 duniani.

    Ndani ya kipindi cha mwka mmoja uliopita,Rwanda ilitekeleza marekebisho matano,na kurahisha ufanyaji biashara,haswa katika biashara nbdogo na za kati.

    Miongoni mwa marekebisho hayo ni pamoja na kuboresha mchakato wa kibali cha ujenzi kwa kuongeza ukaguzi na udhibiti wa ubora.

    Mchakato huo awali ulichukua muda mrefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako