• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Serikali yatoa mpango wa kifedha wa kuboresha upatikanaji wa huduma

    (GMT+08:00) 2017-11-01 19:27:58

    Serikali ya Uganda imewahakikishia wananchi kuwa mkakati wa Kitaifa wa Ujumuishwaji wa Kifedha wa mwaka 2017-2022 utapunguza idadi ya watu ambao hawako katika mfumo wa kifedha kwa asilimia 10 katika miaka mitano ijayo.

    Maafisa wanasema mkakati huo unatoa mfumo wa muda mrefu kwa ajili ya uafikiaji wa maono ya "Waganda wote kupata ,na kutumia,huduma mbalimbali za kifedha,bora na za bei nafuu ,ambazo zinasaidia kuhakikisha usalama wao wa kifedha".

    Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mkakati huo jijini Kampala,Gavana wa Benki Kuu ya Uganda Emmanuel Tumusiime Mutebile alisema wizara ya fedha,mipango na maendeleo ya kiuchumi pamoja na Benki ya Uganda ziliamua kuunda mkakati huo wa kitaifa ambao unalenga kupunguza ambao hawajajumuishwa katika huduma za kifedha kutoka asilimia 15 hadi asilimia 5 mwaka 2022.

    Aliongeza kuwa lengo kuu la kuimarisha ujumuishwaji wa kifedha ni kuboresha hali za wananchi wa Uganda na kuchangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako