• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Russia

    (GMT+08:00) 2017-11-01 20:06:15

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri mkuu wa Russia Dmitry Medvedev.

    Rais Xi amesema Russia ni nchi jirani iliyo kubwa zaidi na ni mwenzi wa kimkakati kwa pande zote wa China, na China haitabadilisha lengo na nia yake ya kuendeleza na kukuza uhusiano kati ya nchi hizo mbili. China inapenda kushirikiana na Russia kupanua ushirikiano wao katika sekta zote, na kuongeza uratibu na ushirikiano katika mambo ya kimataifa, na kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja duniani.

    Bw. Medvedev amesema mkutano mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China umetoa mpango mkuu kuhusu maendeleo ya China katika siku zijazo, ambao una maana kubwa kwa China na dunia nzima. Russia inapenda kufanya mawasiliano na ushirikiano wa karibu zaidi na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako